MBINU ZA KUMPATA MSICHANA MZURI BILA YA KUMHONGA PESA BALI YEYE AKUPE PESA WEWE

Mjue msichana mzuri/mrembo na tabia zake kwa wanaume wanaomtongoza.

Siku hizi wasichana wengi wazuri yaani warembo kuwapata lazima uwahonge pesa nyingi kama hutatumia mbinu utakazofundishwa kwenye  mafunzo haya ya mapenzi, ukitaka hata msichana wa kulala nae siku moja tu lazima utatumia pesa nyingi kumshawishi akukubalie kukupa penzi. Jamii imebadilika sana si kama zamani ambapo mapenzi yalikuwa hayaangalii una pesa kiasi gani, Mapenzi yalikuwa yanaangaliwa kwa upendo wa dhati jinsi mtu anavyokupenda na malengo yake kwako. Siku hizi msichana ukimtongoza hata kama unaonana nae kwa mara ya kwanza barabarani atakukubalia kwa maneno hapo hapo na kukupa namba ya simu kama umemwomba .

Usidhani amekukubalia kwamba wewe ni mzuri sana au umemvutia kwa umbo au kwa maneno uliyompa lahasha subiri dakika tu mkishapeana kisogo halafu uangalie sms zitakazo anza kuingia toka kwa mwanadada huyo aliyekupa namba. Utakuta  sms kama baby naomba nisaide pesa kidogo babu yangu anaumwa sana nataka nikamwone kijijini,  tena anakuambia nitumie kwa simu, maskini ya mungu pengine babu yake anayesingizia anaumwa alishafariki miaka kumi iliyopita lengo ni kuanza kukulia pesa zako tu, ukisha tuma hizo pesa za kwenda kumtazama babu yake kesho utasikia “naomba nitumie pesa kidogo nilikuwa nadaiwa  chuo sikumaliza ada”umeshakuwa mzazi wake sasa lakini angalia unaweza usiambulie hata kumgusa chuchu.

Ataendelea hivyo hivyo akikuomba pesa ndogo ndogo mpaka siku unashangaa umefikisha milioni halafu ukimwambia mbona unazidi kuniomba pesa tu halafu sioni kama umenikubali kweli basi naomba tufanye mapenzi utasikia atakachokuambia na utabaki unaduwaa atakuambia maneno yanayo endana na haya “ vipesa vyako vinakuuma ehee,kama vinakuuma nipoteee chukua time yako” Hapo hazungumzii kukurudishia hela  alizokula yani ameshakutenda hapo utabaki unawaza bora hizo hela ulizokuwa unamsaidia ungefugia kuku wa nyama pengine ungekuwa na biashara kubwa.

Ndivyo walivyo wasichana wengi hawana fadhira kwa wanaowapenda kwa dhati. Mwanaume akimpenda binti  ataweza kula mkate wa shilingi mia nne huku akishushia na maji ili tu huyo msichana apate pesa zitakazomwezesha kufanya anachotaka. Mwanaume furaha yake ni kukubaliwa na kupewa penzi toka kwa binti huyo lakini mabinti wengi wakifanyiwa wema huwa hawakumbuki mpaka siku wakisha pewa mimba na kukataliwa na waliowapa mimba ambao nao walimhonga pesa nyingi akachanganyikiwa akidhani  pesa nyingi ndiyo upendo mwingi ,kumbe asijue wapo wanaume ambao wao kuhonga milioni ili wafanye mapenzi na mwanamke ni kitu kidogo kwao kwani pesa wanazo lakini wanaume kama hawa walio wengi huwa hawana mapenzi ya dhati. Sasa binti akishamwona  bosi ana kazi nzuri anadhani hapo ndio pakutegesha  mimba ili aolewe tena hata bila ya kufanya utafiti kama huyo anayemtegeshea  mimba ana mke au hana mke.

Wanaume wengi wamedhurumiwa sana penzi na pesa zao. Wapo waliowasomesha mabinti toka sekondari mpaka chuo  kwa lengo la kuwaoa lakini binti akishahitimu chuo na kupata kazi anamsahau aliyemtoa mbali mpaka kumfikisha hapo anamwacha mwanaume huyo tena kwa matusi juu. Sasa kama binti wewe hukumpenda mwanaume huyo kwanini ulipokea pesa zake tena kwa kudai na kumnunia wakati mwingine ili tu atoe pesa?  Mwanaume alikutegemea kukuoa asilimia zote ndiyo maana akakusikiliza kwa kila shida uliyomwambia leo unamwacha hivi hivi hali akiwa amekugharamia pesa nyingi sana.

Uzuri wa msichana huyu unamfanya atongozwe kila siku na watu tofauti tofauti kwa hiyo wewe kijana wa kiume ukisha anza uhusiano na msichana huyu mzuri lazima  atakufanya umsikilize kwa kila kitu atakachokisema na ukikosea kidogo tu mfano amekuomba shilingi elfu ishirini kwenda kusuka nywele bahati mbaya siku hiyo ukawa hauna na ukamwambia ukweli kuwa leo sina, basi hapo hapo atachukulia ndiyo sababu na kuanza kukutumia ujumbe mfupi wa dharau na kukuambia “nipotezee kama hutaki kunipa hiyo hela basi kaa nayo” Japo anajua ametumia hela zako zaidi ya laki lakini leo kukosa elfu ishirini tu anatuma ujumbe wa kuonesha hakutaki eti humjali sasa utabaki unajiuliza kama ningekuwa simjali binti huyu ningemgharamia hela zote nilizomsaidia awali? Hutapata jibu na utabaki unalalamika moyoni kuwa bora nisingempa hata shilingi huyu binti na hela hizo ningewasaidia maskini ili Mungu anizidishie thawabu. Wasichana kama hawa tunawapa sifa ya ziada kuwa wana roho mbaya sana ndio maana Mungu anawapa adhabu ya kutoolewa na kulea watoto peke yao kwa tabu maishani mwao. Dhuruma si zuri hata kidogo. Binti ukiamua kula hela ya aliyekupenda basi kubali kuwa naye maishani labda mwanaume huyo awe yeye ndio chanzo cha kuachana  na sio kumtafutia sababu zisizo za msingi ili umwache kwakua umeshamfilisi pesa nyingi sasa unataka usiolewe ili uendelee na tabia hiyo ya kuwalia pesa wanaume.

Hivi ndivyo walivyo wasichana wengi siku hizi hasa hasa hawa waliojaliwa kuwa na shepu nzuri sura nzuri na rangi ya kumvutia mwanaume.

Tafsiri ya msichana mzuri ipo tofauti kwa wanaume mbalimbali, wapo wanaotamani wanawake kwenye makalio makubwa wenyewe wamewapa majina ya mtaani ya utani hapa ndipo wasichana wanaingia maduka ya kichina kupata matako makubwa kama hawakujaliwa kuwa nayo. Wanaume wengine wanavutiwa na wasichana wembamba tu hata kuwafanya baadhi ya akina dada wale mlo moja kwa siku na kujisababishia vidonda vya tumbo ili wawanase wanaume wanaovutiwa na sifa hii, wengine wanavutiwa na miguu minene wenyewe wanaita wasichana wenye miguu ya bia. Wapo wanaovutiwa na wanawake wenye ngozi isiyo nyeusi hapa ndipo panapowafanya akina dada waichukie ngozi nyeuzi na kuanza kujichubua hadi wanaharibu uzuri wa asili waliombiwa na mwenyezi Mungu. Kila mwanaume kuna kitu anachovutiwa sana kwa mwanamke aliyemtamani. Wanaume wachache wanamtafusiri msichana ni mzuri kutokana na tabia aliyonayo kutokana na kutanguliza matamanio ya ngono badala ya kufikiria msichana huyu atakuwa faida namna gani maishani au atakuwa mzigo ndani ya nyumba.

Karne hii mshichana mzuri wa sura na umbo akiolewa basi amshukuru Mungu kwani wengi hawaolewi kutokana na tabia zao hizo mbaya za kudhani Mungu aliwapa uzuri ili wautumie kuwalia pesa vijana wa kiume na kuwatelekeza. Wasichana hawa wenye sura nzuri na maumbo ya kuvutia huwa wanajisahau kuwa kadili siku zinavyozidi kwenda uzuri wao unachuja, wanadhani watabaki wazuri na watawavutia wanaume mpaka wanapoingia kaburini. Wanawaletea nyodo vijana wanaotaka kuwaoa hatimae mwisho wanajikuta wameshika mimba zisizotarajiwa na kuzalia nyumbani kwa wazazi tena wakikataliwa na waliowapa ujauzito kwakuwa tayari wana wake zao au wana wasichana waliowapenda wasioangalia kiasi cha pesa wanazopewa bali wanaangalia wamependwa vipi na mwanaume huyo.

Sasa utabaki unajiuliza kwanini msichana mzuri mrembo amepewa mimba halafu amekataliwa  na kuacha ahangaike kulea mtoto peke yake kwanini asimwoe binti mzuri huyu awe pambo la nyumba? Jibu ni tabia mbaya. Msichana mzuri anajivunia uzuri kuwa anawavutia wengi mtaani kwahiyo kwake tabia nzuri haoni kama ni kitu cha msingi katika maisha ya kuishi na mume. Wengine wanajidanganya eti bora kuishi peke yao bila mume ili wawe huru kumbe hawajui wanawatesa watoto wao kisaikolojia kutokana na  kupata malezi ya mzazi moja na kukosa malezi ya baba. Pia kiuchumi familia zenye mzazi moja zina kipato kidogo ukilinganisha na familia zenye  wazazi wote  wawili  kwani ikitokea mama ameugua na akashindwa kuwatafutia watoto mahitaji muhimu basi baba ataziba pengo hilo.

Zipo sababu nyingi zinazowafanya mabinti siku hizi kuzalia nyumbani bila kupata bahati ya kuolewa ikiwemo  hizi  kuu

1.Tabia mbaya: Kutomuheshimu  mwanaume aliyemtongoza toka siku ya kwanza anapoanza uhusiano hii ni kudhani uzuri wake ni siraha tosha itakayo mfanya aolewe. Mwanaume anamchunguza tabia binti toka siku ya kwanza anapomtongoza sasa kama binti ataonesha kuwa na tabia mbaya mwanzoni kabisa huyu mwanaume anaweza badilisha mawazo ya kuoa na kuishia kumchezea tu.

2. Kupenda pesa sana: Toka siku ya kwanza anaombwa urafiki na kupeana namba za simu yeye ni kueleza shida zake za hela tu na hata kununa asipopewa hela. Mwanaume huwa anaweka rohoni kitendo hiki na kuwaza muda mwingi kwamba huyu binti hata nikimwoa siku nikikosa pesa atanivumilia? Jibu lake anajikuta anaishia kufanya mapenzi na binti ikitokea mimba mwanaume huyu anaikataa kwani anawaza akioa siku akikosa pesa atanuniwa  sana na hata pengine kunyimwa chakula cha usiku.

3. Kuwa na Marafiki wengi wa karibu wa kiume : Kutokana na uzuri wa huyu binti  na kuwavutia vijana wengi basi yeye anachofanya ni kuwa na marafiki wengi wa kiume ili akiamua leo aombe pesa kwa Abdala kesho kwa Hamis keshokutwa kwa John na hata siku moja anaweza omba kwa wote  mara moja ili apate pesa nyingi anunue simu ya gharama nae aonekane kuwa ana hela na maisha mazuri. Kwahiyo siku zinanavyozidi enda kati ya hawa wanaume akigundua kuwa huyu binti ana wanaume wengine anao wasiliana nao kama yeye hawezi kuwa na lengo la kuoa tena kwani anajua mchezo huu hautaishia kwenye uchumba tu bali utaendelea hata wakioana.

4. Tamaa: Binti hata apewe nini bado haridhiki, anatamani apewe kingine na mwanaume mwingine. Ana tama ya vitu, akidanganywa kidogo tu na mwanaume mwingine anamkubalia huyo pia mwisho anawakosa wote wakigundua huyu binti si wa mmoja bali ni wa wote kutokana na tamaa aliyonayo.

5. Ongeza ya kwako kwenye koment “leave reply” hapo chini

Uzuri wa mwanamke wa kuoa ni tabia na sio vitu vinginevyo. Unaweza mtamani mwanamke mzuri wa sura ukamwoa ukadhani umepata faraja masihani kumbe umepata matatizo maishani mwako kwani unapotoka kazini kuelekea nyumbani unaanza kukucha uso na kununa mara tu unapowaza kuwa sasa naenda nyumbani kwa mke wangu.

Sio wasichana wazuri wa sura wote wana tabaia mbaya na roho mbaya au wanapenda pesa tu bali walio wengi wao wanatabia mbaya kwakua wananuchukulia uzuri wao kama fimbo ya kuwapigia wanaume wanaompenda msichana kutokana na sura na umbile hivyo wanaufanya mwili wao kuwa kiegauchumi cha kujipatia pesa.

Zipo mbinu za kumtongoza binti mrembo bila hata ya kumhonga pesa bali wewe unayetongoza utampata kimapenzi na atakupa pesa kama anazo. Hata kama unataka starehe ya siku moja tu kwa binti huyo utapata bila ya kumhonga kiasi chochote cha pesa. Hauhitaji kuwa na sura ya mzuto kwani mabinti wengi sura kwa mwanaume ni sifa ya ziada. Vipo vitu ambavyo ukivijua baada ya kusoma mafunzo haya mpaka mwisho shida yako ya kukataliwa na wasichana kimapenzi na tatizo la kuliwa pesa tu pial hata kufanya nao mapenzi litakwisha kabisa. Wengi wametumia mbinu hizi na kutoa ushuhuda kuwa zimewasaidia wengine wameoa mabinti wazuri wa sura tena na mahali wamelipiwa na binti badala ya wao kuhangaika kutafuta pesa ili wakalipe mahali kwa wazazi. Utampata msichana wa aina yoyote utakayo tena bila kusumbuliwa kupigwa kalenda miezi hata mwaka.

Ndugu msomaji uandaaji wa mafunzo haya unatumia gharama kubwa sana na hatuwezi kuogopa gharama kama kweli tuna lengo la kuelimika na kuielimisha jamii yetu sasa tunaomba utoe mchango kidogo kusaidia kuyafanya mafunzo haya yawanufaishe watu wengi zaidi.

Tunaomba uchangie shilingi elfu moja tu kwa Tigo namba 0652428852 Kisha tuma neno “mapenzi” Kwenda namba hiyo hiyo hapo hapo utatumiwa password na utaingiza hapo chini ili uendelee kufuatia na kusoma mafunzo haya ya mbinu za kutongoza bila kuhonga pesa  mpaka mwisho. Pia password hiyo hiyo utaitumia kusoma Vitabu vya mahaba vinavyoandikwa na watalamu wa masuala ya mapenzi na kuwekwa kwenye mtandao huu.

Ukiwa na swali  au unatafuta mpenzi weka app ya wasapu kisha jiunge na group la Mapenzi Mubashara bonyeza hapa

Kama umeshapata password basi itumie kufuatilia mbinu zote hapa chini kila siku Karibu sana Unaweza download App ili mafunzo haya uyafuatilie kwenye simu yako ya smartphone Download App kwa kubonyeza hapa


One thought on “MBINU ZA KUMPATA MSICHANA MZURI BILA YA KUMHONGA PESA BALI YEYE AKUPE PESA WEWE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *