Askari alivyo niokoa ugenini | simulizi-Mkasa
- InUncategorized
- By support
- July 18, 2021
Askari alivyoniokoa ugenini | simulizi-Mkasa
Siku moja binti mmoja niliyetokoea kumpenda sana alikuja kunitembelea nyumbani kwangu, ilikuwa siku ya furaha sana kwangu, Huyu binti hakika nilikuwa nilishampenda sana tangu siku nyingi zilizopita, Binti wa kiafrika mwenye rangi nzuri ya kuvutia ya kiafrika, binti huyu nahisi ni bikra kutokana na tabia nzuri aliyo nayo, niliwaza kimoyo moyo.
Binti alifurahi kupaona nyumbani kwa mara yake ya kwanza, nilimtembeza kila kona ya mazingira yetu mpaka bondeni tuliko fugia samaki, aliyapenda mazingira na kunipongeza ubunifu mkubwa wa kuchimba mabwawa ya samaki hayo. Nilimwambia kwetu kitoweo cha samaki hakikosekani, tukihitaji tu kula samaki tunakuja bwawani tuna vua samaki idadi ya kututosha tunawaandaa kwa kitoweo. Binti alitamani maisha hayo, tulizunguka sehemu zote na baadae akasema anataka kuondoka nimsindikize basi sikuwa na papara ya kuanza kumbembeleza alale hata siku moja tu nyumbani ndo aondoke. Nilimchumia machungwa akaweka kwenye mkoba wake tukaanza safari ya kurudi kumbe alikuwa…. Inaendelea……
mgonjwa na alikuwa anakuja kuniaga aende kutibiwa gonjwa linalomsumbua huko nchi ya nje, tuliendelea na mazungumzo akinionesha njia aliyopita wakati wa kuja huku nikishangaa aliijuaje hii njia wakati Mimi sijawahi kuipita, binti huyu tulikutana sehemu ya kazi yaani tulikuwa tunafanya kazi wote wilaya moja ya mkoa wa mpakani kigoma ndiko hisia za mapenzi zilipoanzia.
Basi nilimsindikiza kama kilomita 2 tukivuka mabonde yenye uoto wa asili mzuri na na milima iliyotuzwa vizuri na wananchi wa nchi hiyo ya Kongo, tukiwa tumefika mpakani mwa Tanzania na Kongo nikaendelea kumsindikiza kilomita chache mbele na kumuaga aendelee na safari bahati nzuri kulitokea na Dada mwingine anayefahamiana naye wa nyumbani kwakwe ambaye waliambatana nae.
Kabla hajaanza kwenda alipigiwa simu na mama yake huku nikisikiliza, Mwanangu unaendeleaje, umefika wapi? Donda lako vipi? Nikashikwa na wasiwasi kwa maana mpenzi nimpendae alikuwa ananificha ficha ugonjwa anaoenda kutibiwa huko Kongo, Mama alimaliza kuzungumza nae na kukata simu kumbe nikagundua binti haishi na mama kwasababu binti ameajiriwa wilaya tofauti na walikozaliwa, niliwaza kimoyo moyo akirudi ntakuwa naenda kwake hadi kulala huko hata siku zote za wikiendi siku ambazo hatuendi kazini.
Binti alisema nimeweka laudi spika ili uamini naenda Kongo kutibiwa kidonda changu cha tumboni kisha akapandisha brazia na kunionesha kidonda kibichi pembeni ya kitovu chake kizuri na mavuzi yakionekana kwa chini.
Nilisikitika kuona vile na kumtamani yani maeneo anayonionesha lakini sikuwa na jinsi ya kukiponya kile kidonda wala kutoa mawazo mengine tofauti na kuendelea na safari ya kwenda Kongo, nikaamua sasa nimkodie boda boda ya Kongo nililipia sh elfu mbili na kumpa pesa kidogo ya kumsaidia huko aendako tukaagana wakaendelea na safari na rafiki take.
Mimi sasa nikawa narudi mdogo mdogo kupita Yale mabonde yote na milima yenye uoto mzuri wa asili na sauti za ndege wa kuvutia sasa nilikuwa nachunguza vizuri na kufaidi utalii huu nchini Kongo mpakani na tanzania. Wakati narudi nilikuta vijinjia vya mnyama adimu ndezi vingi sana vimekatiza njiani nilitamani ningekuwa Kongo ningewatega wale ndezi kwakua ni kitoweo kizuri. Kwetu uruguruni Morogoro tulishawawinda ndezi wote kwa kuchoma moto milima na mabondeni na kuwakimbiza na mbwa wawindaji pamoja na kuwatega mitego kwenye njia zao wanazopita ndezi hao hadi sasa huwezi pata nyama ya ndezi Tanzania kirahisi rahisi labda uingie maeneo ya hifadhi za wanyama pori na huko hakuingiliki kizembe sababu askari wa wanyama pori wapo kila sehemu na ni wakali sana.
Nikawaza cha kufanya ili niweze kuwa nawafaidi wale ndezi waliokuwa wanashambulia mpunga na miwa mashambani upande wa Kongo huku Mimi nikiwa naishi kigoma. Nikamuuliza mkongo mmoja nilikutana nae njiani eti hapa kuna sehemu ya kupata chakula maana njaa ilikuwa imenishika akanionesha njia nikaenda, nilishangaa kuona kuona hoteli ya kifahari maeneo hayo ya porini mpakani mwa Kongo na Tanzania. Nilihudumiwa na wadada wazuri wa Kongo nikala nikanywa na kuendelea na safari. Sasa wakati nakaribia geti LA mpakani nikakutana na wakongo kama saba hivi wanakuja Tanzania kimagendo kufanya shuguli zao bila vibali, nikawaza kimoyo moyo hawa watanisaidia kupata wale wanyama ndezi wa Kongo tena nitawakamata wazima wazima ili niwafuge Tanzania kwakua Tanzania ndezi anatoweka kabisa.
Niliamua kuwasalimia wale vijana nao wakaanza kunichangamkia kwakua walijua nitakuwa msada kwao tukifika Tanzania nchini kwangu. Nikawauliza nyie wakongo mnawezaje kutunza mazingira kiasi hiki? Uoto wa asili unaonekana upo wa miaka mingi yani hamchomi chomi misitu moto. Wakanijibu sisi wakongo tunathamini sana mazingira, tulirithi utamaduni huu toka kwa mababu zetu, Na huwa tunatumia mila za kusema kwenye msitu huu kuna Joka kubwa lina vichwa saba hivyo ukiingia na kukata miti au kuchoma moto linakumeza kabla hujaanza uharibifu huo, Hizi imani turirithi na sisi tunarithisha watoto na wajukuu ndio maana unaona misitu hii na mapori haya hayaharibiwi.
Nikawaeleza azma yangu kuwa nimeona kuna ndezi wengi huku kwenu kama pale naona wamekula miwa shambani Leo Leo usiku natamani ningekuwa mkongo nifaidi kitoweo hiki kitamu cha ndezi. Wakanijibu hata sisi wakongo tunawala hawa ndezi lakini kutokana na kutunza mazingira wanazaliana sana ndio maana hawaishi kama nyie huko Tanzania. Mnawawinda hadi kwa kutumia moto matokeo yake mnachoma watoto wa ndezi waliozaliwa kwakua hawawezi kukimbia majanga ya moto pia mnachoma ndezi wakubwa ambao watashambuliwa na moto pande zote walipojificha kwenye kichaka.
Nikasema kati yenu naweza pata namba za simu au za watu wa maeneo haya ya mpakani lakini wawe wanaishi Kongo ili niwe naleta mitego ya kuwakatamata wazima wazima siku wanapokuwa wameingia kwenye mtego napigiwa simu nakuja kuwachukua, walinisaidia kuniunganisha na mkulima mmoja aliyekuwa anafanya shuguli zake za kilimo pale mpakani nikaanza kushirikiana nae kwa kupanga cha kufanya tukabadilishana mawazo na kupeana mawasiliano sasa tumefika getini mpakani askari wa Kongo hawa hapa wapo wawili wakatuuliza uraia ikaonekana Mimi sina kibali na uraia wa Kongo nilijitetea nimemleta mgojwa Kongo Mimi sio mtu mbaya wale askari walifoka sana nilikaa pale kama nusu saa kuna askali mgambo mmoja wa kongo ailikuwa akinihoji sana na kunitania pombe za kienyeji za tanzania ambazo aliwahi kuzinywa mkoani kigoma tukaongeaongea pale wakaniruhusu, wale wakongo kama saba waliaomba ruhusa ya kuja Tanzania kutembea nje ya mpaka wakiongopa watarudi siku hiyo hiyo, askari wa Kongo wakawasachi kama hawajabeba siraha au pesa za Kongo wakawaachia wavuke geti, nami walinisachi kila sehemu kama sina kitu kilichozuiriwa kuvuka mpaka. Tukavuka geti, huku nawaza sasa hao ndezi nitakuwa nawavushaje hapa maana ndezi ni Mali asili kama tembo na meno yake ukikamatwa ni jera miaka yote mpaka unafia huko.
Huku tunaendelea na safari ya kuja Tanzania nikawaza nitaweka urafiki na askari wa Kongo ili waniruhusu kuvusha ndezi toka Kongo hata kwa kuwapa ndezi kadhaa maana ni kitoweo kizuri najua watakipenda na Mimi kuniachia angalau ndezi dume watatu na ndezi jike saba wa kufuga ili nisiendelee na ujangili nisije siku moja kukutana na askari wasiokubali kuvusha ndezi wakaniweka chini ya ulinzi na kunipeleka gerezani bila mazungumzo.
Pia niliwaza kuwa nikianza hiyo kazi ya kukamata ndezi Kongo nitaanza na kutengeneza mazingira na askari wa mpakani Kongo kwanza wakikataa Basi nitaacha lakini niliwaza mambo yakiwa magumu askari wakikataa nitatoa wazo langu hili la ufugaji wa mnyama ndezi kisomi zaidi na kupata kibali serikalini hii haitasumbua maana serikali ya Tanzania ikinielewa itanisaidia kwa kupata huyu mnyama ndezi bila vikwazo, sababu serikali ina uwezo wa kupata ndezi kupitia sekta ya mifugo na sekta ya wanyama pori lakini niliwaza hivi na udogo wangu huu sina cheo sina pesa nitaishinikiza serikali inisaidie ikanielewa?
Hapo mazungumzo mengine na wale wakongo yakiendelea na safari inaendelea taratibu sasa tulikuwa tumechoka tulifika sehemu moja Tanzania kama kilometa 1 toka getini mpakani Kongo tukapumzika chini ya mwembe. ilikuwa msimu wa embe, tuliangua embe na kula ghafla gali la police vuuu nipo na wakongo wale saba….
Akili haraka nikaanza kuwaza nitajiteteaje hapa Mimi moja kwa moja nitaonekana ndo nasafirisha hawa wakongo, wakati wala siwajui kwao wala wanakokwenda huu msala naepukaje “wote mpo chini ya ulizi piga magoti, piga magoti Tutawamaliza leo” askali walinda mipaka walitoa amri.
Tulipiga magoti wote kimya tukifokewa na askari wale “nyie majambazi eti.. mnatafuta nini hapa sura zenu ni wakongo mna vibali vya kuja Tanzania?” Wote tupo kimyaa hakuna wa kujibu mara kofi teke , kabla sijafikiwa na kipigo alitokea askari mgambo wa Kongo ambaye nilikuwa nimejitambulisha kwake kuwa Mimi ni mtendaji kata huku Tanzania kumbe wala nilimwongopea tu ile asubuhi pale getini ili anione ni mtu fulani mwenye wadhifa serikali ya Tanzania huyu mgambo alikuwa ameitwa kwa ajili ya kutafsiri lugha kwa wale watu saba wa kongo.
Askari wa Tanzania walidhani hawa watu hawajui kiswahili maana walikuwa wakihojiwa hawajibu kumbe wale wenzangu waliamua kuanzisha vurugu kupambana na askari polisi waliotukamana mara wakongo wakachukua mawe kutishia polisi ili wapate mwanya wa kutoroka polisi wakaona hakuna haja ya kufyatua risasi waliwamudu kwa ngumi mitama.
Mimi nilitulia kimya ile wamemaliza majibizano ya mapambano wakawa wanakuja kunikamata na Mimi kinifunga pingu maana walihisi tu mimi sio mkongo kutokana na taaluma yao na nilivyotii amri yao ya kupiga magoti na kutulia, ndipo mgambo yule wa Kongo akamtonya askari mmoja wa Tanzania Kisiri siri lakini nilisikia kwa mbali anachomwambia kuwa msaidieni huyo alikuwa amesindikiza mgonjwa wake kutibiwa Kongo Leo Leo alipita getini pale tukamruhusu na ndio alipokuwa anarudi alikutana na hawa wakongo wenzangu na kuambatana nao mpaka hapa… Na story imeishaaaa
Story hii inatufundisha mambo mengi kama kutunza mazingira, kuonesha upendo, maswala ya rushwa, unaweza komenti kingine ulichojifunza pengine hata wengine hawajakigundua.. Comment hapa chini.