Habari za muda huu, Hongera kwa kuwa online kujifunza mambo mapya kila siku. teknolojia imekuwa sana na inaendelea kubadilika kila kukicha sasa usipojifunza vitu vipya utabaki na umaskini wako na utapitwa na mengi.
Leo hii unajifunza jinsi unavyoweza kutengeneza pesa kwa kutumia whatsapp yako uliyoizoea kila siku. Whatsapp ni mtandao unaomilikiwa na mmiliki wa facebook ambaye anaitwa Mark Zuckerberg Huyu jamaa sasahivi ni Tajiri mkubwa duniani na alianza na facebook aliyoigundua akiwa chuo, story yake inavutia sana ndugu huyu. Alikuwa amepewa kazi ya kufanya kama group pale chuoni yaani watengeneze mtandao wa kuunganisha wanachuo wote wa chuo alichokuwa anasoma yeye badala ya kutia nguvu kwenye kazi hiyo ya group anakawa anatengeneza mtandao wake kumbuka kazi zote alikuwa akifanya chumbani kwake bwenini. Mara akafanikiwa kubuni mtandao wa facebook ambao kwa mara ya kwanza aliupa jina la facemash. Mtandao huo ulipokelewa vizuri na wanachuo na ukaanza kusambaa kwenye vyuo vingine duniani ikiwemo vyuo vya tananzania badae wananchi wengi wakaupata na kuufurahia.
Hivi ndivyo bwana Mark Zuckerberg alivyo anza safari yake ya mafanikio kwa kuunda facebook, Aliingiza pesa nzuri kwa mtandao huo na badae akaanza kununua mitandao mingine kama whatsapp and akaongeza instagram ili aongeze watumiaji. Kadili watumiaji wanavyokuwa wengi ndivyo anavyoingiza pesa nyingi kwa njia ya matangazo ya kulipwa. Ugunduzi huu ulianza mwaka 2004 na kijana huyu mdogo wa kipindi hicho hata mika 25 alikuwa bado hana aliamua kuacha masomo yake na kufungua kampuni. Kumbe watu wanasoma ili wapate pesa na sio elimu. Hata wewe leo ukiwa chuoni ukapata milioni 100 unaweza kuacha chuo na kuanza biashara lakini sikushauri elimu ni ufunguo wa maisha kadiri unavyopata elimu zaidi ndio unaiwezesha funguo yako kufungua mlango wowote wa mafanikio.
Whatsapp ina watumiaji wengi sana, Kila mwenye smartphone ana whatsapp kwenye simu yake. na siku hizi watu wengi wanamiliki simu za smartphone na wengine wanaipata whatsapp kwakutumia kompyuta. Sasa hii ni fursa kwako kutengeza hadi laki 3 kwa mwezi kwakutumia whatsapp hapa unaifunza hatua kwa hatua mpaka uanze kuingiza pesa kwa whatspp
Mafunzo haya siku za mbeleni watu watalipia sh 1900 kuja kusoma hapa lakini wewe unapewa ofa ya kusoma bure kama utabonyeza tweet au share hapo kwenye kibox makala hii itafunguka na utaisoma hakikisha umeituma kwenye twitter yako au facebook yako Ukibonyeza tweet hakikisha una sign in na kuirusha twitter ukibonyeza share to facebook hakikisha umeenda mkapa mwisho habari iende facebook hapo hapo utaona kibox hapo chini kimefunguka na utasoma hatua zote bure
Asante kwa kushare sasa unaweza kuendelea kujifunza.
Kuanza kutengeneza pesa kwa whatapp kwanza jiulize una kitu gani ambacho ukiwashirikisha watu watakipenda mfano wakati unajiuliza angalia umesomea nini? je ni kilimo, mifugo, maendeleo, mwalimu, daktari? kwakifupi fani yako au ujuzi wako ukishajua sasa jiulize swali jingine je hiyo fani ukiibadili kuwa huduma ambayo utaitoa kwenye whatsapp je watu wataipenda na kuwa tayari kulipia?
Pili andaa mada zako kama ni kufundisha kilimo sawa, kama ni kufundisha ufugaji sawa, kama ni kufundisha kutengeneza keki sawa, mapishi sawa chochote kile ambacho unahisi watu watakihitaji na watakuwa tayari kulipia pesa kidogo.
Tatu, Fungua group whatsapp kisha lipe jina zuri linaloendana na kile utakachokuwa unafundisha mfano kama utakuwa unafundisha ufugaji tumia jina kama ufugaji bora, mfungaji tajiri, tajirika kwa ufugaji na majina mengine kama hayo ambayo yanavutia watu kujiunga.
Nne sasa ni hatua ya kuanza kutengeneza pesa, Ndio hii biashara unaanza kutengeneza pesa toka siku ya kwanza umefungua group. Kuna njia mbili za kuwaleta wateja kwenye group moja unaweza sambaza link ya group kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, telegram na watsapp yenyewe ukiwashawishi watu kujiunga lakini waambie kabisa kubaki kwenye group lazima walipie. Sasa mtu akishajiunga kwenye group unamfuata inbox na kumwambie alipie kabla mafunzo hayajaanza kwa siku hiyo kama hajalipia ikifika muda wa mada husika ya siku unamtoa kabla hujarusha mafunzo yako. kwakua namba yako tayari atakuwa nayo pale whatsapp akitaka kuiunga atakutumia ujumbe wa kuhusu kulipia na utamuunga kwenye group tena. Usikasirike ukiona mtu halipii si wote wana pesa leo mwingine hana leo lakini kesho atakuwa nayo na atalipia.
Nia ya pili ni kuficha link ya group yaani huitangazi popote bali unatangaza kwa maeno na kuwaambiwa tu watume namba zao uwaunganishe na unaweka kiwango cha pesa. Tunashauri usitoze pesa nyingi anza na hata sh 500 kwa mwezi ili kuvutia watu kujiunga. group la whatsaap lina uwezo wa kujaza members 250 sasa ukipata watu 250 utakuwa na sh 125000 kwa mwezi ndugu yangu hii pesa si ndogo ukilinganisha na muda unaotumia kufundisha mada zako kwa mwezi.
Njia zote hizo ukiona unashindwa kupata members wa kujiunga whatsapp basi unashauriwa kulitangaza group lako kuna watu wamebobea katika online marketing wanauwezo wa kukuletea watu 250 kwa siku na kujaza group lako. wasiliana nao https://www.twitter.com/jamiihuru watakutangazia group lako kwenye account za twitter zenye followers zaidi ya 120000 kwa sh elfu 15 tu hapo hukosi members 250 kwa siku.
Mambo muhimu ya kuzingatia unapoendesha huduma hii.
Kila kitu kina hitaji umakini hata hii biashara inahitaji umakini na utakutana na vikwazo lakini usikate tamaa mfano utakutana na watea wanakutukana usijibu matusi, Mjibu vizuri hata akutukanaje hakuharibii maisha yako. mtu mbaya ni anayekukata mkono kwakua una mikono hata wakutukane wewe piga kazi utafanikiwa.
Mwisho usimtapeli mtu, jambo baya huwa linaenea kwa haraka kuliko jambo nzuri ndio maana baadhi ya watu maarufu huwa wanafanya mambo mabaya maksudi ili kuamusha mashabiki wao wawafuatilie halafu baada ya muda kidogo wanatoa wimbo au movie. Hivyo usimtapeli mtu kwa kupokea pesa halafu usimhudumie. Pia kumbuka siku hizi simu zetu zinachungwa na wenye nchi kwahiyo unajulikana hadi mnara wa simu unaotumia hapo mtaani.
Hongera kwa kusoma mpaka mwisho sasa umefudhu kuanza biashara hii nzuir, Fanya zoezi usiipuuzie biashara hii, nawashauri wanachuo mmesomea vitu vingi sana lakini mnabaki mnazunguka navyo kwenye mabahasha kutafuta kazi wakati una uwezo wa kuanzisha ofisi yako mtandaoni kama nilivyokufundisha hapa.
Kama mafunzo haya umeona yanafaida kwa vijana basi share link hii fursa.jamiihuru.com ili na wengine waje wajifunze hapa, umaskiini sasa basi.[
Nimeshare
Ila still bado haifunguki
Inafunguka bila shida hakikisha umeshare vizuri na post imeenda kwenye facebook au twitter au whatsapp